tangazo

Virusi vya corona: Kwanini mahitaji ya kununua mahandaki duniani yameongezeka

                 handaki hili linalojengwa nchini Ujerumani ndilo linalotarajiwa kuwa kubwa zaidi dunian
Larry Hall na Robert Vicino, waanzilishi wa kampuni mbili maalum za kujenga na kuuza mahandaki ya kujivinjari au majumba yaliojengwa chini ya ardhi nchini Marekani hawakuwa na fikra kwamba huenda biashara yao ikanoga.
Katika vichwa vyao walifikiria kuhusu uwezekano wa shambulio la Korea Kaskazini ama kuanza kwa vita vya dunia vya tatu.
Katika miaka ya hivi karibuni wamejenga mahandaki ya chini ya ardhi na kuweka milango ya vyuma mbali na faraja zote wanazohitaji wateja wao kuokoa maisha yao kwa miezi michache ama miaka.
Na sasa wafanyabiashara wote wawili wanadai kwamba mahitaji ya mahandaki yao yameongezeka kwa hofu ya mlipuko wa virusi vya corona na wanadai kupokea simu nyingi kwa siku kutoka kwa wateja.
Ukweli ni kwamba sio kila mtu ana uwezo wa kulipia huduma kama hii.
Vivo ambayo ni kampuni ya Roberto Vicino inauza mahandaki hayo kwa $40,000.
Upande mwengine mahandaki mengine yenye faraja ya hali ya juu yanauzwa kwa gharama ya hadi $4.5m.
Majumba haya yaliotengenenezwa chini ya ardhi yapo barani Ulaya nchini UjerumaniHaki miliki ya pichaVIVOS
Image captionMajumba haya yaliotengenenezwa chini ya ardhi yapo barani Ulaya nchini Ujerumani
Handaki la Vivo halikujengwa na saruji na milango ambayo ina uwezo wa kuzuia risasi . Ni mpango mwengine wa kuokoa maisha na kuendelea kuishi.
''Ni Jumba ambalo halihitaji mtu kutoka nje kwa mwaka mmoja'', Dante Vicino ambaye ni msanifu wa majumba aliambia BBC Mundo.
Vivo inajivunia mahandaki katika miji ya Indiana na Kusini mwa mji wa Dakota, nchini Marekani pamoja na majumba mengine makubwa barani Ulaya nchini Ujerumani.
Hanadaki lililotangazwa nchini Ujerumani kupitia mtandao wake litakuwa handaki kubwa zaidi litakapokamilishwa.
Wanalilinganisha na jahazi la mtume Noah na kusema kwamba kila familia itaweza kufurahia nafasi ilio zaidi ya mita 200.
Baadhi ya vifaa vinavyopatikana katika mahandaki hayo ni pamoja na Vidimbwi vya kuogelea, maeneo ya kufanyia mazoezi na maeneo ya kutazama filamu.
Wamiliki wake wataweza kuwasili kwa kutumia magari ama hata ndege za kibinfasi karibu na uwanja wa ndege ulio karibu, kama ilivyoahidiwa katika mtandao wake.
''Ni mahandaki ya kuzuia bomu la kinyuklia ambayo yameundwa kwa muundo wa kuwalinda wamiliki wake kimwili na kiakili'' , alisema Larry Hall, mmiliki wa kampuni ya Survival Condo katika mahojiano na BBC 2017.
Mahandaki hayo yamewekwa vifaa vya kuingiza hewaHaki miliki ya pichaVIVOS
Image captionMahandaki hayo yamewekwa vifaa vya kuingiza hewa
Pia aliweza kuelezea kwamba amwetumia mamilioni ya madola kujenga nyumba zilizopo katika hali kama hiyo ili kuishi ndani yake kwa kipindi cha muda mrefu.
Katika nyumba hizo kuna mifumo ya kuchuja hewa na maji, chanzo cha kawi mbadala , vidimbwi vya kuogelea , maeneo ya kutazama filamu, maeneo ya kufanya upasuaji mbali na walinzi watakaolinda milango ya nyumba hizo.

Mahitaji yameongezeka

Katika siku za hivi karibuni , wananuzi wanaotaka kununua nyumba hizo za ardhini wameongezeka.
lakini sasa wito ni tofauti.
Wanunuzi wanahofu kuhusiana na mlipuko wa corona kulingana na Hall.
''Kile ambacho washauri wa jela hufanya, wataalam wanaowashauri watu matajiri wakati wanapokwenda jela , wanataka kujua idadi ya mahandaki yaliosalia na bei yake'', anaongezea.
Mfanyabiashara huyo anasema kwamba mnunuzi mmoja hivi karibuni alinunua mojawapo ya handaki bila ya kulitembelea na kuliona lilivyo.
''Alitupigia simu , tuliandaa ziara yake na baada ya siku nne alinunua nyumba hiyo ya chini ya ardhi''.
Survival Condo.Haki miliki ya pichaSURVIVAL CONDO
Image captionSurvival Condo ilijenga muundo wa kipekee wa jumba la chini ya ardhi mjini kansas Marekani
Hatahivyo msukosuko unaohusishwa na virusi vya corona haubagui na pia unawaathiri wale wanaoweza kuishi katika mahandaki. Wengi wa wateja hawako katika nafasi ya kununua.
Kwanza wanahitaji soka la hisa kuimarika ama hata kuuza mali fulani ili kuweza kununua nyumba hizo za ardhini.
''Inakera kwasababu hatuwezi kufadhili kila mtu'', anasema Hall. Vicino pia naye anasema kwamba wateja wameongezeka.
Hatahivyo anasema kwamba wateja wake sio matajiri pekee, lakini hata watu wa uchumi wa wastani wamewasiliana naye kuhusu nyumba hizo.
''Wateja wetu sio kwamba wanapendelea sana kuishi katika mahandaki lakini ni wateja wasomi ambao wanataka kuzificha familia zao wakati wa mlipuko huu'', anaelezea Vicino.
Baadhi ya huduma zilizopo ndani ya majumba hayo ya chini ya ardhi ni michezo ya kujifurahishaHaki miliki ya pichaSURVIVAL CONDO
Image captionBaadhi ya huduma zilizopo ndani ya majumba hayo ya chini ya ardhi ni michezo ya kujifurahisha
''Huu ni mpango mbadala wa wateja ambao wanataka kujificha kwa kuwa wanahofia kwamba ulimwengu utapasuka kutokana na tisho la ugonjwa, shambulio la Korea kaskazini ama vita vya tatu na Urusi na China'', anasema Vicino.
Analinganisha umiliki wa hanadaki na ule wa gari ama bima ya maisha.
''Unadhania unalipia kitu usichohitaji, lakini utakihitaji unapokihitaji''.
Survival Condo.Haki miliki ya pichaSURVIVAL CONDO
Image captionMahandaki ya kujivinjari kulingana na wasimamizi wake huwekwa vifaa ambavyo vitamfanya anayeishi ndani yake kusalia humo kwa miezi michache na hata mwaka mmoja


Post a Comment

0 Comments