tangazo

NEC yakamilisha zoezi la uhakiki wapiga kura Zanzibar

Tume ya taifa ya Uchaguzi ya Tanzania NEC imekamilisha zoezi la uhakiki wa wapiga kura kwa upande wa NEC Visiwani Zanzibar huku hali ya tahadhari ya ungonjwa wa Corona ikizingatiwa kwa mawakala na wananchi wanaofika vituoni kwa ajili ya uhakiki wa taarifa zao katika daftari la kudumu la mpiga kura.

Licha ya janga la maradhi ya Corona hali hiyo haikuwa kikwazo kwa wananchi kufika katika vituo vya uhakiki kama ambavyo ilitarajiwa.

Afisa usimamizi wakituo hiki cha Kwa-Alinatu chenye majimbo matano Abdull Azizi Ame Hilali anasema zoezi hilo limekamilika kwa wakati kutokana na uelewa wa wananchi na utayari wao wakuitumia haki ya kujiandikisha.

Post a Comment

0 Comments