tangazo

Mahakama ya Ufaransa yaamuru Kabuga ashtakiwe nchini Tanzania

Felix in Kabuga ndiye aliyekuwa mtu tajiri zaidi nchini Rwanda kabla ya mauaji ya 1994.

Mahakama nchini Ufaransa imeagiza Félicien Kabuga ambaye anatuhumiwa kuhusika na mauaji ya kimbari ya Rwanda kufikishwa mbele ya mahakama maalum ya Umoja wa mataifa iliopo Tanzania.
Mwanabiashara huyo wa Rwanda anakabiliwa na mashitaka ya kufadhili na kuchochea mauaji ya kimbari ambapo waendesha mashitaka wanasema alifadhili makundi ya Kihutu ambayo yaliwaua karibu watu 800,000 kutoka kabila la Watutsi mwaka 1994.
Kabuga, mwenye umri wa miaka 87 alikamatwa viungani mwa mji wa Paris mwezi uliopita baada ya kuwa mafichoni zaidi ya miaka 25.
Amekanusha mashitaka dhidi yake na kuyataja kuwa ya uwongo.

Mawakili wa Kabuga wanasema, Kabuga anataka kushtakiwa nchini UfaransaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMawakili wa Kabuga wanasema, Kabuga anataka kushtakiwa nchini Ufaransa

Wiki iliyopita waendesha mashitaka wa mahakama ya kimataifa kwa ajili ya Rwanda waliomba kwamba kesi dhidi ya Kabuga ifunguliwe mjini The Hague kwa hoja kwamba Arusha Tanzania kuna tishio la ugonjwa wa virusi vya Corona lakini pendekezo hilo lilitupiliwa mbali na jaji mkuu wa mahakama hiyo Bwana William H.Sekule


Bw. Kabuga anaweza kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa kuhamishia kesi yake katika mahakama maalum ya Umoja wa Mataifa, iliyo na makao yake mjini Arusha Tanzania na mjini Hague Uholanzi).

Je Filicien Kabuga ni nani?


Félicien Kabuga, alikuwa mtu tajiri zaidi Rwanda, alitumia utajiri huo kutoroka kukamatwaHaki miliki ya pichaEPA
Image captionFélicien Kabuga, alikuwa mtu tajiri zaidi Rwanda, alitumia utajiri huo kutoroka kukamatwa

Ndiye aliyekuwa mtu tajiri zaidi nchini Rwanda kabla ya mauaji ya 1994.
Akijipatia utajiri wake kupita biashara ya majani ya chai mwaka 1970 na alifanya biashara katika sekta chungu nzima nyumbani na katika mataifa ya kigeni.
Alikuwa mshirika wa karibu wa chama tawala cha MRND - na alikuwa na uhusiano na rais wa zamani Juvenal Habyarimana ambaye alifariki 1994.
Akituhumiwa kwa kuwa mfadhili mkuu wa mauaji hayo na kutumia biashara yake na uwezo wake kupanga na kufadhili mauaji.
Mmiliki wa kituo cha redio ya kibinafsi RTLM alishutumiwa kwa kuwachochea watu wa kabila la Hutu kuwaua Watutsi.
Mwaka 2006, jopo la kimataifa la Rwanda lililokuwa likichunguza mauaji hayo lilisema lina ushahidi kwamba bwana Kabuga alizuru nchini Kenya ama hata kuishi nchini humo, ambapo alikuwa akisimamia maslahi yake ya kibishara.
Miaka mitatu baadaye, Bwana Stephen Rapp, ambaye alikuwa balozi wa Marekani aliishutumu serikali ya Kenya kwa kukataa kumtoa bwana Kabuga.Kulikuwa na ushahidi kwamba bwana Kabuga alihudhuria hafla zilizoshirikisha watu maarufu, alisema madai ambayo Kenya imekana.
Ni wazi kwamba familia ya bwana Kabuga ilikuwa ikimiliki mali nchini Kenya baada ya mali moja kuzongwa na kesi 2015 wakati mkewe, Josephine Mukazitoni , ambaye alikuwa mmiliki mwenza , alipojaribu kumiliki.

Post a Comment

0 Comments